Home BUSINESS ANZANIA YAKUBALIANA NA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA KUUNDA MFUKO WA KUKABILIANA...

ANZANIA YAKUBALIANA NA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA KUUNDA MFUKO WA KUKABILIANA NA WANYAMA WAKALI NA WAHARIBIFU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Mawaziri kutoka Botswana, Zimbabwe, Zambia na Namibia, katika Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo (kulia) na Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Kay Kagaruki wakifuatilia Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na Mawaziri kutoka Zambia na Botswana wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa (hayupo pichani) akifungua rasmi Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Mawaziri kutoka Zambia na Botswana wakiagana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa (kushoto) baada ya kufungua rasmi Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika kwenye Hifadhi ya Hwange nchini Zimbabwe

HWANGE ZIMBABWE.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeingia makubaliano na Nchi za Kusini mwa Afrika kuunda mfuko maalum kwa kila nchi wa kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu hususan tembo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja(Mb) katika Kongamano la Tembo wa Afrika lililofanyika leo katika Hifadhi ya Taifa Hwange nchini Zimbabwe.

“Tumekubaliana kwamba kuwepo na mfuko maalum kwa kila nchi ambao utakuwa mahsusi kwa ajili ya kudhibiti wanyama wakali na waharibifu kama tembo na pia kuwezesha wananchi wanufaike na rasilimali wanyama hao” Mhe. Masanja amefafanua.

Ameongeza kuwa mfuko huo utakapoanzishwa utawanufaisha wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi na waathirika wa wanyama hao wanaoumizwa au kuuawa kwa kuwezesha kulipwa fidia .

Mhe. Masanja amesema kuwa sambamba na hilo mkutano huo umelenga kuangalia namna jamii zinazoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi kuangalia namna zinavyoweza kushirikishwa katika kutunza rasilimali za wanyama hususan tembo.

Aidha, amesema nchi hizo zimekubaliana zisiingiliwe katika maamuzi na nchi za Magharibi kwa kuwa zenyewe ndio zinahusika katika kutunza wanyama hao na pia zinazoathirika na changamoto za wanyama hao.

Kongamano hilo  limehudhuriwa na Mawaziri na Maafisa Waandamizi kutoka nchi za Botswana, Namibia, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

Previous articleJENGO LA HUDUMA ZA DHARURA TABORA LAKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA JUMATATU
Next articleTAULO ZA KIKE 1000 ZAKABIDHIWA, VIJANA WAFUNDWA HEDHI SALAMA KINYAMWEZI SEKONDARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here