Home LOCAL MEYA KUMBILAMOTO AWAPONGEZA JIJI KWA HATI SAFI

MEYA KUMBILAMOTO AWAPONGEZA JIJI KWA HATI SAFI

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto akimkaribisha Mkurugenzi wa jiji hilo Jumanne Shauri katika futari iliyoandaliwa na Meya Jana, (Katikati) Diwani wa kivukoni Sharik Choughule (Picha na Heri Shaaban).
Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na Watendaji wa hamashauri ya jiji hilo wakila futari iliyoandaliwa na Meya wa jiji Omary Kumbilamoto jana (Picha na Heri Shaaban)

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto (Picha na Heri Shaaban).

Na: Heri Shaaban (ILALA).

MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam  Omary Kumbilamoto amewapongeza Watendaji ,Wakuu wa Idara na madiwani kwa kupata hati safi miaka sita mfurulizo.

Meya Kumbilamoto aliyasema hayo Dar es salaam  jana wakati alipoandaa futari katika mfungo wa Ramadhani  ambayo amewafuturisha wakazi wa Dar es salaam , madiwani wa Halmashauri ya Jiji na  wafanyakazi wa Jiji. 

“Ninawapongeza madiwani wangu kwa usimamizi wa miradi vizuri pamoja na Watendaji wa Halimashauri ya Jiji awali (ILALA )kwa usimamizi mzuri wa miradi kupelekea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka sita mfurulizo ” alisema Kumbilamoto.

Aliaema hati safi wameanzia  kupata 2014/2015/2016, /2017, /2018, /2019, /2020  yote hiyo kutoka na kazi nzuri ambayo inafanywa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji na Watendaji wake.

Aliwataka Watendaji wa halmashauri ya Jiji hilo madiwani kushirikiana kufanya kazi ili kuisaidia Serikali ifikie malengo yake katika kujenga TANZANIA ya uchumi wa viwanda.

Aliwataka wakazi wa Dar es salaam kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassani katika kuchapa kazi

Aidha aliwapongeza Benki ya CRDB kwa ushirikiano wao mzuri ndani ya halmashauri hiyo ya Jiji  kuunga mkono Juhudi, za Serikali sekta ya Elimu pamoja na kuleta maendeleo.

Mwisho

Previous articleRC KUNENGE AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA WANANCHI DAR, MUFTI WA TANZANIA ATOA NENO.
Next articleRAIS SAMIA KUTARAJIWA KUWA MGENI RASMI BARAZA LA IDDI MWAKA HUU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here