Home LOCAL IDARA YA UHAMIAJI YAWASIMAMISHA KAZI ASKARI WAKE WATATU.

IDARA YA UHAMIAJI YAWASIMAMISHA KAZI ASKARI WAKE WATATU.

DAR ES SALAAM.

Idara ya uhamiaji Tanzania imewasimamisha kazi watumishi wake watatu kwa tuhuma za kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao.

Askari hao wamesimamishwa kazi kwa kutenda kosa la matumizi ya nguvu kinyume cha sheria dhidi ya mtuhumiwa wa utapeli Alex Kyai kufuatia picha za video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha tukio hilo.

Katika taarifa iliyotolewa leo Mei 30 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Anna Makakala imesema kuwa Idara yake imesikitishwa na kitendo hicho kilichofanywa na askari hao.

“Idara ya uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo hicho kilichofanywa na askari wa uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao. Hata hivyo idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya skari hao” Amesema Kamishna Jenerali Makakala.

Aidha ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe kwenye Ofisi za Uhamuiaji.

Pia amewahakikishia wananchi wote kuwa Idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weledi, uwazi na bila kutumia mtu wa kati (Vishoka),  na kuomba kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hii.

“Natoa Onyo kwa mtu yeyote ambaye atajaribu kujifanya Afisa wa Uhamiaji au Afisa yeyote wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslai yake binafsi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake” Amesisiza Kamishna Makakala.

Mnamo tarehe 27 Mei 2021 Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli  ndugu Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji kurasini Dar es Salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za Pasipoti aliyemtambulisha kama mkewe. Baada ya mahojiano ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata Pasipoti kwa haraka. Pia mtuhumiwa amekuwa akijitambulisha kama mtumishi wa Taasisi nyeti ya Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Shushwa (TAKUKURU)

Previous articleJESHI LA POLISI MKOA WA KAGERA LAENDELEA NA UCHUNGUZI NA KITU KILICHODAIWA NI BOMU KUWALIPUKIA WATOTO
Next articleTANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO 30 VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU, VIKWAZO VINGINE 34 VIPO KWENYE MKAKATI WA UTEKELEZAJI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here