Home LOCAL WADAU SEKTA YA ULINZI WAPEWA ELIMU

WADAU SEKTA YA ULINZI WAPEWA ELIMU

Kamishna wa Kazi Msaidizi Ukaguzi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rehema Moyo akitoa elimu ya utekelezaji wa sheria kwa wadau wa sekta ya ulinzi binafsi nchini katika ukumbi wa Karemjee hall Jijini Dar es salaam katika semina ya mafunzo ya sheria za kazi kwa wadau wa ulinzi binafsi nchini.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina ya mafunzo ya sheria za kazi iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu kupitia idara ya kazi

Kamishna wa Kazi Msaidizi Ukaguzi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rehema Moyo akitoa elimu ya utekelezaji wa sheria kwa wadau wa sekta ya ulinzi binafsi nchini katika ukumbi wa Karemjee hall Jijini Dar es salaam katika semina ya mafunzo ya sheria za kazi kwa wadau wa ulinzi binafsi nchini.

Na: Mwandishi wetu, Dar es salaam

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi, imetoa elimu ya sheria za kazi kwa Wafanyakazi na Waajiri wa sekta za ulinzi leo Septemba 4, 2024 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Kamishna wa Kazi wa Ofisi hiyo, Suzan Mkangwa amesema sekta za ulinzi zimekuwa na malalamiko yanayotokana na ukiukwaji wa sheria za kazi, hivyo elimu waliyoitoa itasaidia kuondoa changamoto zilizopo.

Aidha, Mkangwa amebainisha baadhi ya malalamiko ambayo yamekuwa yakiripotiwa ofisini kwake ikiwemo wafanyakazi kuajiriwa bila mikataba, Waajiri kutowasilisha michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuachishwa kazi kiholela bila kuzingatia sheria za kazi.

Ni matumaini yangu semina hii itakwenda kuondoa changamoto za ukiukwaji wa sheria za kazi ambazo zimekuwa zikiripotiwa ofisini mara kwa mara” amesema.

Awali akizungumza Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Asha Udindo ametoa rai kwa Waajiri wa sekta hizo kujiunga WCF na kuwasilisha michango kwa wakati ili kulinda haki zao dhidi ya majanga yanayoweza kuwapata wafanyakazi wao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.

Naye, Meneja Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Dar es salaam Feruzi Mtika amesema Serikali haitawavumilia waajiri wote wa sekta binafsi ambao wanakata michango ya wafanyakazi wao bila kuiwasilisha katika Mfuko huo.

MWISHO

Previous articleAJALI USAFIRI MAJINI ZAPNGUA GEITA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here