Home LOCAL MHE.DKT PHILIP AMEWASILI NCHINI LESOTHO

MHE.DKT PHILIP AMEWASILI NCHINI LESOTHO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho Mhe.Neo Matjato Moteane wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mashoeshoe Mjini Maseru nchini Lesotho leo tarehe 04 Oktoba 2024. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. James Bwana wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mashoeshoe Mjini Maseru nchini Lesotho leo tarehe 04 Oktoba 2024. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mashoeshoe Mjini Maseru nchini Lesotho leo tarehe 04 Oktoba 2024. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mfalme wa Lesotho Mfalme Letsie III katika Ikulu ya Kifalme iliyopo Maseru nchini humo. Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Lesotho. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.

Previous articleRC MALIMA AWATAKA WATAALAMU WA MISITU SUA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA UHIFADHI WA MISITU
Next articleTCU YAONGEZA MUDA WA UDAHILI WANAFUNZI ELIMU YA JUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here