Home LOCAL RC SENYAMULE: MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA MTUACHIE ALAMA WANADODOMA 

RC SENYAMULE: MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA MTUACHIE ALAMA WANADODOMA 

Mkuu wa mkoa  Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza leo Septemba 23,2024 jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.
Na WAF-DODOMA
Jumla ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Rais Samia wapatao 50 wamepokelewa mkoani Dodoma na Mkuu wa mkoa  Mhe. Rosemary Senyamule na  kuwataka kwenda kuwahudumia watanzania wa mkoa huo kwa siku zote sita watakazokuwepo kwenye Halmashauri zote nane za mkoa huo kwa moyo wa Upendo na kuacha kumbukkumbu hata wakiondoka.
Mhe. Senyemule ameyasema hayo Septemba 23, 2024 wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.
Tunataka mtakapo ondoka muacha alama kwa wananchi lakini pia watumishi ambao kwa namna moja au nyingine mtakuwa mkishirikiana nao bega kwa bega muda wote na kuwajengea uwezo mkoani kwetu kwenye Halmashauri zote nane” amesisitiza  Senyamule.
Mhe. Senyemule amesema wanafarijika kuona uwekezaji mkubwa uliofanya na Serikali upande wa miundombinu ya afya na sasa wanapelekewa Madaktari Bingwa na Bobezi kwa ajili yakutatua changamoto za afya kwa wananchi wa ngazi ya msingi. 
Zamani Madaktari Bingwa ungeweza kukutana nao kwenye Hospitali maalum hasa zile zilizojulikana kama za Kanda lakini pia taifa lakini leo, Mabingwa ninyi mnashuka hadi kwenye ngazi ya Halmashauri kwa ajili yakushughulikia afya za watanzania, kipekee nimshukuru sana Rais Samia  kwa maono yake ya kujali na kuwasogezea wananchi Huduma za afya karibu,” ameongeza Mhe. Senyamule 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Kaspar Mmuya amesema ujio wa Madaktari Bingwa ni fursa kwao na kama ingekuwa ni mapendekezo yake basi wangeendelea kubakia katika mkoa wao ili wanachi waendelee kupata Huduma hizo kila mara.
Akitoa salama za wizara Dkt. Mathew Mushi kutoka Wizara ya Afya ameeleza kuwa  malengo ya zoezi hilo  ni muendelezo wa kambi ya awamu ya kwanza iliyofanyika kwa mafanikio ambapo wananchi zaidi ya 70,000 waalifikiwa na Huduma hizo za ubingwa na bingwa bobezi.
Katika awamu hii shabaha nikuwafikia wananchi 100,000 kwa huduma zote tutakazozitoa kwenye Halmashauri 184 kote nchini” amesema Dkt. Mushi”, na kuongeza
Madaktari waliopokelewa ni pamoja Upasuaji, Usingizi, Watoto na wanawake Madaktari wa kinywa na Meno, Magonjwa ya ndani pamoja na Wauguzi Mabingwa na Wabobezi.

Mkuu wa mkoa  Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza leo Septemba 23,2024 jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya,akizungumza wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.

Sehemu ya Madaktari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa  Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) ,akizungumza leo Septemba 23,2024 jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.

Mkuu wa mkoa  Mhe. Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwapokea  Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.

 

Previous articleMHE.RAIS ALAKIWA KWA SHANGWE NA VIGELEGELE, AKIANZA ZIARA RUVUMA
Next articleMHE.BASHE ATOA BEI ELEKEZI YA MAHINDI RUVUMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here