Home LOCAL DKT. TULIA AKUTANA NA RAIS WA INDIA AKIHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI HUMO

DKT. TULIA AKUTANA NA RAIS WA INDIA AKIHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI HUMO

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, tarehe 24 Julai, 2024 amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini India kwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Droupadi Murmu Ikulu Jijini New Delhi.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Tulia amewasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuishukuru na kuipongeza Serikali ya India kwa kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kijamii baina ya nchi hizo mbili.

Dkt. Tulia amebainisha kuwa ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia aliyoifanya nchini humo mwaka 2023 imeongeza chachu ya kukuza uhusiano kwa kuleta manufaa katika sekta za afya, elimu, ulinzi na maji.

Vilevile, Dkt. ameipongeza nchi hiyo ambayo ni Mwanachama wa Kundi la Nchi 20 (G20) kwa kupigania maslahi ya Afrika katika kundi hilo na kubeba ajenda ya kufanya mabadiliko ya uwakilishi ulio sawa katika Umoja wa Mataifa.

Mara baada ya mazungumzo hayo, Dkt. Tulia pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bunge (Upper House) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Jagdeep Dhankhar ambapo pamoja na mambo mengine amelipongeza Bunge hilo kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za IPU, kutunga Sheria ya kuongeza idadi ya uwakilishi wa Wabunge wanawake Bungeni kwa kufikia asilimia 33 pamoja na kupitisha Bajeti yenye kulenga kuinua uchumi na kipato cha vijana, wanawake na makundi maalum.

Previous articleRAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
Next articleTRA SHINYANGA YASIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPA KODI DIDIA & PUNI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here