Home BUSINESS JAJI MKUU: BRELA NA MAHAKAMA ZIUNGANISHWE KWENYE KANZIDATA MOJA

JAJI MKUU: BRELA NA MAHAKAMA ZIUNGANISHWE KWENYE KANZIDATA MOJA

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameitaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuiwezesha Mahakama nchini kuunganishwa kwenye Kanzidata ya Wakala ili kuweza kuhakiki taarifa za kampuni kwa uharaka pindi inapokuwa inashughulikia mashauri yahusuyo kampuni hizo

Rai hiyo ameitoa leo tarehe 5 Juni, 2024 alipotembelea banda la BRELA lilipo ndani ya jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam.

Mhe. Prof. Ibrahim Juma amesema kuwa uunganishwaji katika kanzi data itaiwezesha Mahakama kujua uhai wa kampuni na endapo imehuisha taaifa zake kwa Msajili hii itasaidia kuamua kuendelea na kesi au kusitisha endapo kampuni haijahuisha taarifa zake kwa Msajili

Aidha, Jaji Mkuu ameipongeza BRELA kwa kazi kubwa inayofanya katika kuboresha utoaji wa huduma zake kwa njia ya mtandao

BRELA inashiriki katika kutoa huduma za papo kwa hapo kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam ndani ya banda la Wizara ya Viwanda na Biashara na banda karibu na Wizara ya Fedha na Mipango

Previous articleTAWA YANADI FURSA ZA UWEKEZAJI MAONESHO YA 48 YA KIMATAIFA ALMAARUFU SABASABA 2024
Next articleRAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA BIASHARA CBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here