Home BUSINESS HUDUMA ZA BRELA ZA MTANDAO ZAPUNGUZA VISHOKA

HUDUMA ZA BRELA ZA MTANDAO ZAPUNGUZA VISHOKA

DAR ES SALAAM 

Huduma za mfumo wa kimtandao zilizoboreshwa na Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (BRELA), zimewawezesha wananchi wengi kupata huduma hizo na kuondoa kwa kiasi kikubwa changamoto ya vishoka.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wananchi waliofika katika Banda la BRELA kupata huduma zinazotolewa kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akiongea kwenye mahojiano maalum Jacob Mwakasoye mkazi wa mbeya amesema mfumo wa kimtandao wa BRELA unakwenda kumaliza malalamiko ya wananchi hususani suala vishoka waliokuwa wakiwatapeli pesa zao.

“Kwakeli huduma za BRELA za mwaka 2012 na sasa ziko tofauti sana, kwani sasa wameboresha huduma zao kupitia mfumo unaomsaidia mwananchi kufanya Usajili yeye mwenyewe” alisema Mzee Mwakasoye ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Mbeya.

Naye Emmanuel Mishapiti mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), amesema BRELA imemuwezesha kusajili jina la Biashara katika sekta ya Utalii ambayo ndio fani anayosomea.

“Tumefanikiwa kusajili jina la Biashara ya fani tunayosomea ya Utalii, na Baadae tutasajili Kampuni itakayotuwezesha kufanya kazi zetu kwa ufanisi zaidi” amesema Mishapiti.

Kwa upande wake Afisa Usajili wa BRELA Koyan Ndalway Aboubakar amesema kuwa katika maonesho hayo zaidi ya wananchi 150 wamehudumiwa na kupewa vyeti vyao vya Usajili papo kwa hapo, ambapo ametoa rai kwa wananchi kuacha kuwatumia vishoka na badala yake kutumia mfumo wa kimtandao ili kupata huduma za BRELA.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yanafikia tamati leo Juni 23, na yameongozwa na Kauli Mbiu isemayo “KUWEKEZA KWA UTUMISHI WA UMMA WA AFRIKA KARNE YA 21 ILIYO JUMUISHI NA INAYOSTAWI; NI SAFARI YA MAFUNZO NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA” ambapo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma.

Previous articleNHC INAVYOKWENDA KUGEUZA ENEO LA URAFIKI KISASA 
Next articleKAMPUNI YA DRAFCO YAUSHUKURU UONGOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here