Home Uncategorized NEMBO YA SWAHILI FASHION WEEK 2021 YAZINDULIWA RASMI

NEMBO YA SWAHILI FASHION WEEK 2021 YAZINDULIWA RASMI

 


NA: MWANDISHI WETU.

Balozi wa Italy nchini Marco Lombardi, amezindua nembo ya msimu wa 14 wa tamasha la mitindo, Swahili Fashion Week ambalo litafanyika kuanzia 3 Desemba mpaka 5 jijini Dar Es Salaam.

Tamasha hili limekuwa likifanyika kila mwaka na kukutanisha wabunifu na wanamitindo kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje ya Afrika 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Balozi amesema nchi ya Italy, ipo sambamba na uongozi wa Swahili Fashion Week kuhakikisha wanafanikisha tamasha hilo kwa mara nyengine.

“Imekuwa ni kawaida ya nchi yetu kudhamini tamasha hili kwa sababu tunatambua sekta ya ubunifu wa mavazi inatoa ajira kwa kasi kwa watu wa rika tofaauti kupelekea na kukuza uchumi wetu,” anasema Marco Lombardi.

Kwa upande wamratibu wa jukwaa hilo Benedict Msofe amesema wabunifu Zaidi ya 50 wamejisaji kuonyesha kazi zao mwaka huu katika tamasha hilo.

“Mwaka huu tumepata muamko mkubwa kwa sababu ya wabunifu wengi wamejitokeza kushiriki katika jukwaa hili kuonyesha kazi zao pamoja na kuzi uza katika hoteli ya Serena ambapo ndipo panapofanyika tamasha hili mwaka huu.

Previous articleHITIMANA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE
Next articleASILIMIA 33 YA VIFO TANZANIA VINASABABISHWA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here