Home BUSINESS TAASISI ZOTE ZA WIZARA WEKENI MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA-DKT. ASHIL

TAASISI ZOTE ZA WIZARA WEKENI MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA-DKT. ASHIL

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk. Ashil Abdallah akizungumza alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Wizaya hiyo Dkt. Ashatu Kijaji leo Novemba 17,2022 Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamisi Livembe akizumguza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi akimkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

PICHA MBALIMBALI ZA WADAU WALIOSHIRIKI MKUTANO HUO.

NA: HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashil Twalib Abdallah ameziagiza taasisi zote zilizopo chini ya Wizara hiyo kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao kwenye mazingira rafiki.

Dkt. Ashil ameyasema hayo leo Novenba 17,2022 kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Wizara pamoja na taasisi zake zina jukumu la kuwezesha wafanyabiashara wote hapa nchini kufikia malengo yao na kwamba kwa kufanya hivyo kutawapelekea wafanyabiashara hao kuweza kulipa kodi ya Serikali bila kushurutishwa.

“Hakuna sababu ya mfanyabiashara kulipa kodi kwa mtutu wa bunduki, tunataka tuwawezeshe wafanyabiashara ili waweze kulipa kodi ya Serikali kwa hiari na urahisi mkubwa” amesema Dkt. Ashil.

Aidha amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa ya kukutana katika mkutano huo kujadiliana kwa kina  na kuainisha changamoto zote zinazowakabili ili Serikali iweze kuzifanyiakazi.

Katika hatua nyingine Dkt. Ashil amewaalika wafanyabiashara hao kutembelea Ofisi za Wizara hiyo siku ya Jumatatu Novemba 21,2022 kuwasilisha changamoto zote walizozijadili kwenye kikao hicho ambapo ameahidi kuzitolea ufumbuzi kwa kushirikiana na Wizara na tasisi nyingine za Serikali kulingana na changamoto husika.

“Nawaomba mkae mzungumze na kujadiliana kwa kina kuzipitia changamoto zote mlizonazo na zile zinazohusu Wizara au taasisi ya Serikali, nawaalika Dodoma Jumatatu ijayo tukae kwa pamoja na kuzipatia ufumbuzi wa pao kwa hapo kwa kushirikiana na wadau wengine” ameongeza Dkt. Ashil.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania Hamisi Livembe ameishikuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kuendelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo na kuweka mazingira wezeshi na kwamba Jumuiya hiyo ina imani kubwa na Serikali ya Rais samia huku wakiamini Changamoto zao zitakwenda kupungua kwa kiasi kikubwa.

Previous articleSAADY KIMJI AMEJITOSA UJUMBE BARAZA KUU WAZAZI TAIFA
Next articleWAZIRI KIJAJI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NCHINI MANFREDO FANTI JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here