Home LOCAL SHILINGI MILIONI 412.4 ZA TASAF KUNUFAISHA ZAIDI YA KAYA 5000- SIKONGE.

SHILINGI MILIONI 412.4 ZA TASAF KUNUFAISHA ZAIDI YA KAYA 5000- SIKONGE.

 

Na: Lucas Raphael,Tabora

Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya Masikini wilaya ya Sikonge mkoani Tabora  imetoa kiasi cha shilingi milioni  412  ikiwa ni awamu ya tatu ya  fedha ambazo zimeanza kutolewa kwa kaya Masikini kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

 

Mratibu wa TASAF Wilaya ya Sikonge Cloud Nkanwa alitoa maelezo hayo kwa waandishi wa habari  katika zoezi la uhawilishaji lililofanyika jana kwa kaya maskini wiayani humo

 

Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni  412.4 zimelenga kuwanufaisha kaya masikini 5758 wanaoishi katika vijiji 64 vilivyopo kwenye  Wilayani hiyo.

 

Cloud alisema kwamba walengwa wa mpango wa kunusuru kaya Masikini wanatakiwa kuzitumia fedha wanazopata kwa malengo yaliyokuwasudiwa, ikiwemo kuwapeleka watoto klinik ,kuwanunulia wanafunzi  sare za shule na mahitaji mengine muhumi ya watoto.

 

Aidha alisema kwamba wanufaika wa mpango huo kuzitumia fedha hizo katika mambo yenye tija ilikuweza kujiinua kiuchumi.

 

“Lengo la mpango huu ni kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato, kuwajengea uwezo na kunusuru kaya Masikini zilizo katika Mazingira hatarishi, jambo ambalo Serikalini imekuwa ikilifanya kwa wananchi” alisema Cloud Nkanwa


Katika hatua nyingine wanufaika wa TASAF ambao ni  Amisa Husein ,Vaines Leonard na Mary Charles  wameishukuru Tasaf  kwa kuendelea kuwapatia fedha ambazo zimewasadia katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha  .

 

“Fedha za TASAF zimenisaidia kufanya Biashara ndogondogo, pamoja na kufuga kuku, na kupitia Biashara  nimejenga nyumba ya Bati ambayo mwanzo sikuwa nayo” Mnufaika wa TASAF.

 

Walisema kwamba Fedha hizo zimelenga kuwawezesha kupata mahitaji ya Msingi na fursa za kujijiongezea kipato kwa njia ya uzalishaji Mali kupitia mpango huo wa  kunusuru kaya masikini na kwa ajili ya manufaa ya muda mrefu.

 

mwisho

 

Previous articleNAIBU WAZIRI KATAMBI AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU ATHARI ZA UVIKO 19 KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZA VIJANA
Next articleTUSIVUNJE MSHIKAMANO WETU KWA MAENDELEO YA TAIFA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here