Home ENTERTAINMENTS KATIBU MWENEZI CCM NDG.SHAKA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MAZISHI YA MSANII MAUNDA ZORRO

KATIBU MWENEZI CCM NDG.SHAKA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MAZISHI YA MSANII MAUNDA ZORRO


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameshiriki mazishi ya Msanii Maunda Zoro, yaliyofanyika Toangoma, Kigamboni Dar es Salaam, (leo) Jumamosi 16 April 2022.

Katika mazishi hayo, Shaka alijumuika na wanafamilia na waombolezaji, ndugu jamaa na marafiki ambapo alipata nafasi ya kuwasilisha salamu za pole na mkono wa rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

”Mhe Rais Samia yuko safari (ziara) amenituma nifikishe salamu zake za pole kwenu ndugu, familia, jamaa na marafiki sambamba na kuwasilisha mkono wa rambi rambi toka kwake, anatambua kuwa tasnia hii imepoteza msanii mahiri ambaye wakati wote wa uhai wake aliitumia Sanaa kufikisha ujumbe , kuburudisha, kuhamasisha na wakati mwingine kuiunganisha jamii kwa ujumbe, sambamba na kuenzi kipaji cha (babake) Mzee Zahiri Zoro lakini Maunda akiwa msanii anaechipukia alifanya vizuri sana”alisema Shaka katika sehemu ya maelezo yake.

Bwana Ametoa , Bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe
Apumzike kwa Amani Maunda Zoro.
Ameen.

Previous articleVISIMA VYA NISHATI YA JOTOARDHI KUANZA KUCHORONGWA SONGWE
Next articleRAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AMEWASILI JIJINI NEW YORK MAREKANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here