Home LOCAL WAZIRI BASHUNGWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI HALMASHAURI YA MVOMERO

WAZIRI BASHUNGWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI HALMASHAURI YA MVOMERO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Bw. Hassani Njama Hassani kuanzia leo tarehe 20.04.2022 ili kupisha uchunguzi.

Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya Tarehe 10.03.2022 Wilayani humo.

Wakati wa ziara hiyo Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa Idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.

Hadi kufikia leo hii hakuna Mkuu wa Idara yeyote ama mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia maagizo hayo.

Aidha Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhifu wa fedha za umma.

Imetolewa na

Nteghenjwa Hosseah

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Rais –TAMISEMI

20.04.2022


Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 20-2022
Next articleWANANCHI MVOMERO WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU WAKATI SERIKALI INATATUA MGOGORO WA MIPAKA YA HIFADHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here