Home LOCAL UBALOZI WA JAPAN KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI ZUZU

UBALOZI WA JAPAN KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI ZUZU

Wakazi wa mtaa wa Mazengo, kata ya Zuzu, mkoani Dodoma, wameliomba shirika la maendeleo la Japan (JICA), pamoja na ubalozi wa Japan, kuwasaidia kuchimba kisima kingine kutokana na kile kilichopo kutokutosheleza mahitaji ya watumiaji kuongezeka.

Kisima kilichopo sasa ni kile kilichokarabatiwa na Japan mwaka 2018 kupitia mradi wa Grassroots, ambao umesaidia zaidi ya wakazi 4,250 kunufaika.

Akizungumza mara baada ya viongozi wa JICA kufanya ziara na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini, Mwenyekiti wa mtaa wa Zuzu, Joshua Kajembe, amesema kuwa kisima hicho kina vituo sita na kwamba watu wengi wanatumia maji, jambo ambalo linafanya maji yasitosheleze, huku uhitaji ukiendelea kuongezeka.

Aidha, amesema kuwa hapo awali kisima hicho kililenga watumiaji 100, lakini sasa watumiaji wanazidi 1,000, hivyo kupata changamoto ya utoshelevu wa maji.

Kajembe ameongeza kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji, wamepanga mgao wa maji katika mtaa huo ili angalau kutosheleza wakazi wote.

Kwa upande wake, fundi wa mradi wa maji wa ukarabati visima katika kijiji cha Zuzu, Emanuel Mdosa, amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu. Amesema tenki la kuhifadhia maji limechakaa na linavujisha maji, hivyo kuhitajika kupatikana kwa lingine.

Naye Kaimu Meneja wa RUWASA Dodoma wilaya, Muhammad Mbanga, amesema kuwa wako kwenye mpango wa kuomba fedha kwa ajili ya kuboresha mradi huo, huku akiomba JICA na Japan kuwaunga mkono katika kutekeleza mapungufu yaliyopo kwa sasa.

Aidha, amesema kuwa huduma ya maji katika mtaa huo ipo kwa asilimia 50, hivyo kudai kuwa bado kunahitajika juhudi za ziada kuboresha mradi huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi wa Zuzu wamesema kuwa uwepo wa mradi wa maji uliofadhiliwa na Japan umekuwa msaada mkubwa kwao, kwani walikuwa wanatafuta maji kwa tabu, ikiwemo wanawake kutafuta maji mbali na kukutana na adha nyingi, ikiwemo za ubakaji.

Wamesema kuwa licha ya uwepo wa mradi huo, bado maji hayapatikani kwa muda wote kutokana na matanki kuwa machache, hivyo kuomba kuongezewa vifaa hivyo ili maji yapatikane saa 24.

Afisa utawala na Mawasiliano JICA TanzaniaAlfred Zacharia akizungumza katika ziara  hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma. 

 

Mwenyekiti wa mtaa wa Zuzu, Joshua Kajembe, akizungumza na waadidhi wa habari katika `ziara  na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini,

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, na waandishi wa habari  wakazi wa Zuzu
 

Fundi wa mradi wa maji wa ukarabati visima katika kijiji cha Zuzu, Emanuel Mdosa, Akitoa maelekezo ya mradi huo  mara baada ya viongozi wa JICA kufanya ziara na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini,

Previous articleBASHE: MADIWANI SIMAMIENI VYAMA VYA MSINGI VISIWADHULUMU WAKULIMA
Next articleTAARIFA YA KAMATI YA SERA YA FEDHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here