Home LOCAL WANANCHI WAFURIKA UWANJA WA MAJIMAJI KUMSIKILIZA RAIS SAMIA RUVUMA

WANANCHI WAFURIKA UWANJA WA MAJIMAJI KUMSIKILIZA RAIS SAMIA RUVUMA

Songea, Ruvuma

Katika hali ya hamasa kubwa, umati mkubwa wa wananchi wa Mji wa Songea umejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Majimaji, kumshuhudia na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 23 Septemba 2024 katika kilele cha Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni, lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mkoani Ruvuma.

Mhe. Rais Dkt. Samia ni mgeni rasmi wa tamasha hilo, lililojikita katika kuonesha na kusherehekea utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Tanzania.

Kabla ya hotuba yake, Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya utamaduni, ambapo alijionea kazi mbalimbali za sanaa na utamaduni, na hata kushiriki kucheza mchezo wa bao, jambo lililowafurahisha wananchi na wasanii waliokuwepo.

Shughuli hiyo inaendelea kwa shamrashamra, huku wananchi wakionesha shauku na furaha kubwa kwa ziara ya Rais katika eneo hilo, likiwa na umuhimu mkubwa kwa historia na utamaduni wa taifa.

Previous articleMHE.BASHE ATOA BEI ELEKEZI YA MAHINDI RUVUMA
Next articleDKT.BITEKO AKUTANA NA UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here