Home LOCAL RAIS SAMIA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUCHOMA MISITU

RAIS SAMIA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUCHOMA MISITU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonya wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu bali wailinde na kuihifadhi.

Ameyasema hayo leo Septemba 26, 2024 katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Acheni kuchoma misitu moto, na kama ni lazima uchome moto shamba linda moto usitapakae kwenda kuharibu maeneo mengine ya misitu yaliyohifadhiwa” amesisitiza Rais Samia.

Amesema wananchi wanapochoma misitu moto inaharibu misitu pamoja na miundombinu ya barabara hivyo inarudisha nyuma maendeleo.

Kuhusu changamoto ya tembo iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Kawawa, Rais Samia amesema changamoto hiyo inaendelea kupatiwa ufumbuzi na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana.

Previous articleDKT.PHILIP AMEWASIHI WANANCHI KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOJENGWA NA SERIKALI
Next articleTANROADS YADHAMIRIA KUBORESHA MIUNDOMBINU NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here