Home Uncategorized RIBA YA BENKI KUU YASALIA ASILIMIA 6

RIBA YA BENKI KUU YASALIA ASILIMIA 6

DAR ES SALAAM 

Riba ya Benki Kuu katika robo ya tatu ya mwaka huu itaendelea kuwa asilimia 6 kama ilivyokuwa katika robo ya pili ya mwaka huu; Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania imetangaza.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kilichofanyika tarehe 4 Julai 2024. Kiasi hicho kimefikiwa ili kutimiza malengo ya kiuchumi katika kipindi hicho, Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila amesema wakati akitangaza uamuzi kwa niaba ya Gavana Emmanuel Tutuba.

Amesema, tathmini ya Kamati kuhusu mwelekeo wa uchumi na vihatarishi mbalimbali inaonesha kwamba utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2024 umefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki chini ya lengo la asilimia 5.

Kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, Gavana Tutuba amesema, Kamati imeridhishwa na kuendelea kuimarika kwa shughuli za kiuchumi, kutokana na utekelezaji wa sera thabiti na maboresho mbalimbali yenye lengo la kukuza uchumi.

Ameongeza kuwa hali ya kuimarika kwa uchumi inatarajiwa kuendelea katika siku zijazo, kufuatia hali ya hewa nzuri kwa ajili ya shughuli za kilimo, upatikanaji wa uhakika wa umeme, uboreshaji wa miundombinu pamoja na sera na programu za maboresho

Riba ya Benki Kuu kwa robo ya nne ya mwaka 2024 itatangazwa mwezi Oktoba mwaka huu . Hii ni kulingana na kalenda ya mikutano ya Kamati ya Sera ya Fedha ya mwaka.

 

Previous articleBENKI YA NMB YAZIPIGA JEKI SHULE MBILI ZA SEKONDARI MKOA WA DAR ES SALAAM
Next articleOREXY GAS YAMTANGAZA SHILOLE KUWA BALOZI WAKE WA UHAMASISHAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here