Home LOCAL HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA YAANZA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI WA MIFUPA

HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA YAANZA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI WA MIFUPA

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila (kushoto) akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imetangaza kuanza kutoa huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa ambayo kwa muda mrefu wananchi wa Shinyanga wamekuwa wakihangaika wanapopata changamoto ya kuvunjika kwa mifupa na kulazimika kusafiri kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Aprili, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila amesema kupitia urafiki wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma wamepata udhamini wa vifaa kwa ajili ya Operesheni ya mifupa kupitia Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma kwa ufadhili wa SIGN Fracture Care International.
 
“Kupitia huduma hii tulipata madaktari bingwa wawili kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma ambao tumekuwa nao tangu Aprili 17,2023 mpaka leo kwa ajili ya kuona wagonjwa wenye shida au changamoto ya mifupa na wengine pia wamefanyiwa Operesheni lakini pia kuwajengea watumishi wenzetu wa Hospitali ya Rufaa Shinyanga kuwa na uwezo wa kufanya hizo Oparesheni za mifupa. 
Sambamba na hayo tuna Daktari wetu Bingwa tulimtuma Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambaye amekaa kwa muda wa mwezi mzima kwa ajili ya kujijengea uwezo wa kufanya Oparesheni za mifupa”, amesema Dkt. Luzila.
Dkt. Luzila ameishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya upatikanaji wa huduma hiyo ya oparesheni ya mifupa katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ili kupunguza changamoto ya wagonjwa kupelekwa Bugando.
Previous articleATAKAYE CHOMA MOTO HIFADHI YA VYANZO VY MAJI JELA MIAKA SABA
Next articleTCRA YATOA MWONGOZO WA KUSAFIRISHA VIFURUSHI NA VIPETO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here