Home BUSINESS DKT. ASHIL AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA VIWANGO DUNIANI JIJINI DAR

DKT. ASHIL AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA VIWANGO DUNIANI JIJINI DAR

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Twalib Abdallah alitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kushiriki kikamilifu katika utayarishaji wa Viwango vya Kimataifa.

Dkt. Abdallah ameyasema hayo tarehe 18 Novemba, 2022 alipomwakilisha Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) katika kufunga maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua Mashindano ya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa Viwango.

Dkt. Abdallah amelitaka Shirika la TBS pamoja na wadau wa uandaaji viwango wametakiwa kuongeza juhudi katika kuoanisha viwango vyetu katika ngazi za kikanda na pia kushiriki kikamilifu katika michakato ya kutayarisha viwango vya kimataifa ili kuwezesha bidhaa za Tanzania kupenya kirahisi katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Hatua hii imewawezesha kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango hatimaye kuwawezesha kupata masoko ya kimataifa.

Aidha amesema kazi inayofanywa na TBS ya kuratibu na kusimamia utayarishaji wa viwango vya kitaifa ni kazi adhimu. Viwango husaidia si tu kufungua mipaka, lakini pia kuhakikisha usalama wa afya na mali, ulinzi wa mazingira na elimu kwa umma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Viwango ya kila mwaka yamelenga kuamsha uelewa miongoni mwa wadhibiti ubora, wafanyabiashara, wenye viwanda na walaji kuhusu umuhimu wa viwango kwa maendeleo ya jamii.

Previous articleMRAJISI MKUU WA VYAMA VYA USHIRIKA DKT NDIEGE AKAGUA MAGHALA YA KUKUSANYA KOROSHO WILAYANI TUNDURU,ATAKA USAWA KWA WATUNZA MAGHALA WALIOTEULIWA ILI KUTENDA HAKI
Next articleJKCI YATOA MILIONI 180 MATIBABU YA WAGONJWA 12 NJE YA NCHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here