Home ENTERTAINMENTS MISS TANZANIA HALIMA AHMAD KOPWE ASHIRIKI UZINDUZI KAMPENI YA UZAZI NI MAISHA...

MISS TANZANIA HALIMA AHMAD KOPWE ASHIRIKI UZINDUZI KAMPENI YA UZAZI NI MAISHA ZANZIBAR

NA: MWANDISHI WETU

MISS Tanzania Halima Ahmad Kopwe ameshiriki uzinduzi wa kampeni ya Uzazi ni Maisha iliyo andaliwa na shirika la Amref Tanzania  pamoja na wizara ya Afya Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa mrembo huyo mbali ya kushinda taji la Miss Tanzania alinyakua taji dogo la mradi ambapo mradi wake ni kusaidia vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua. 

Akizungumza na ukurasa huu amesema hii ni frusa kubwa kwake kwa sababu ni kampeni inayo endana na mradi wake ambao anatarjia kwenda nao shindano la urembo duniani hivyo amewasisitizia watu kuunga mkono kamapeni hiyo.

“Nimefurahi kuungana na kamapuni ya Amref Tanzania na wizara ya afya Zanzibari katika kampeni hii ya Uzazi ni Maisha ni waombe wadau kujitokeza kuungana nasi katika mbio zitakazo fanyika Agost 27, mwaka huu mahusussi kwa kuchangia vifaa tiba kwa uzazi salama,” anasema Halima Kopwe.

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo mke wa Rais wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mariam Mwinyi, amesisitiza kuwa uboreshaji wa afya ya mama na mtoto ni jukumu la kila mtanzania kwani taifa la kesho linategemena na afya ya mzazi wa leo.

Tukio hilo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali Waziri wa afya Zanzibar Mheshimiwa Nassor Mazrui na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga na uongozi wa shirika la Amref Tanzania.

Previous articleFILAMU YA ROYAL TOUR YAENDELEA KULETA NEEMA , WATALII WAZIDI KUONGEZEKA
Next articleMSALABA MWEKUNDU WAFIKISHA SALAMU ZA RAIS SAMIA ZA MKONO WA POLE KWA WAHANGA WA UKAME LONGIDO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here