Home BUSINESS TWCC WAFIKIENI WANAWAKE VIJIJINI: WAZIRI DKT. GWAJIMA

TWCC WAFIKIENI WANAWAKE VIJIJINI: WAZIRI DKT. GWAJIMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, akitoa Hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa Makundi Maalum katika Manunuzi ya Umma kwenye Hoteli Sheraton jijini Dar Es Salaam.


Mwenyekiti wa TWCC Taifa Bi. Mercy Silla akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Waziri Dkt. Doroth Gwajima kuzungumza

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, akizindua Ripoti ya ushiriki wa Makundi Maalum katika Manunuzi ya Umma uliofanyika kwenye Hoteli Sheraton jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, (katikati) akifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa TWCC Mercy Silla alipokuwa akiznungumza. (kushoto) ni, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza.

Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumza alipokuwa akitoa ukaribisho kwa mgeni rasmi na wadau mbalimbali walishiriki Kikao hicho.
 

Baadhi ya Washiriki wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa Makundi Maalum katika Manunuzi ya Umma kwenye Hoteli Sheraton jijini Dar Es Salaam, PICHA NA HUGHES DUGILO.

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka Taasisi ya Chama cha Wanawake wafanya Biashara Tanzania (TWCC), kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kuwafikia wanawake walioko vijijini ambao wamekuwa wakipitwa na fursa mbalimbali kutokana na mazingira yao hali inayo dumaza jitihada za kumkomboa mwanamke.

Dkt. Gwajima, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, Juni, 09, 2022 wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa Makundi Maalum kwenye Manunuzi ya Umma shughuli iliyoandaliwa na taasisi ya Chama hicho.

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekuwa Mstari wa Mbele kuandaa mazingira wezeshi ya kumkomboa Mwanamke lakini fursa nyingi zimekuwa zikibakia kwa wachache waliopo mijini na kundi kubwa ambalo linafikia asilimia kubwa ya uzalishaji mali katika shughuli za kilimo wakibakia bila kuwa na taarifa sahihi.

“Niwaombe ndugu zangu wa TWCC, kwakuwa ninyi tayari mnamtandao mpana uliopo nchi nzima, mtumie fursa hiyo kuwafikia wanawake waliowengi ambao wapo maeneo ya vijijini hawa bado fursa nyingi hawazifahamu hivyo mkitumia vizuri jukwa lenu la TWCC, naimani wengi watapata mwamko na kushiriki katika mambo mbali mbali mathalani haya ya zabuni” amesema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha Wanawake kiuchumi, aidha  uwepo wa mifuko rasmi  ya uwezeshwaji kiuchumi ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), TASAF, Mfuko wa Rais wa Uwezeshaji  na mifuko mingine ni ishara kuwa Serikali inawajali.

Dkt. Gwajima amesema kuwa mwaka 2016 Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka ya Mwaka 2011 katika Kifungu  cha 64 (a) katika kipengele cha 2 kwa kutoa nafasi kwa makundi maalum kuwezeshwa kushiriki katika fursa za manunuzi ya umma iliyotaka  kutengwa asilimia thelathini (30%) ya bajeti yake kwa ajili ya makundi maalum wakiwepo wanawake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa (TWCC) Taifa  Bi. Mercy Silla ameipongeza Serikali na kuomba jitihada hizo ziongezwe kwani wanawake walio wengi wanachukua mikopo wakiwa hawana maarifa ya Biashara au Shughuli wanayotaka kuifanya na hivyo kuishia kufilisika.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha jitiahada za makusukudi kwa vitendo za kutaka kuona wanawake wa Kitanzania  wanajikomboa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutoa fursa mbalimbali zikiwemo mikopo ya Halmashauri

“Mhe Waziri pamoja na washiriki bado ipo changamoto kwa wanawake wanaochukua mikopo ikiwepo masharti yakukopa ambayo husisitiza kuwa kikundi cha watu  jambo hili kwa namna moja linakwamisha jitihada za mtu mmoja mmoja, kwakuwa kila mtu anakuwa na mawazo tofauti hivyo hata wakichukua Mikopo wanashindwa kuelewana, lakini kama masharti yatabadilika itawezesha kila mwenye wazo lake ataweza kufanya anachoweza” alisema Bi. Silla.

MWISHO.

Previous articleMSAMAHA WA MATIBABU HUTOLEWA KWA WATU WASIO NA UWEZO – DKT. MOLLEL
Next articleYONO AUCTION MART
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here