Home SPORTS VINARA WA LIGI KUU YANGA WASHIKWA KOO KWA MKAPA

VINARA WA LIGI KUU YANGA WASHIKWA KOO KWA MKAPA

Na stella Kessy.

VINARA wa ligi kuu  Yanga SC leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Sare inayoiongezea alama moja kila timu, inaifanya Yanga ifikishe pointi 36 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 14.

Mbeya City yenyewe inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Azam FC.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Erick Mwijage dakika ya 20 na 73, wakati la Coastal Union limefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 54.

Kagera Sugar inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 14.

Katika mchezo mwingine ambao  KMC imelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KMC inafikisha pointi 16 katika nafasi ya 10 na Biashara United inafikisha pointi 12 katika nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 14.

Previous articleASKOFU JACKSON SOSTHENES WA ANGLIKANA AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.PILI FEBRUARI 6-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here