Home BUSINESS NAIBU WAZIRI KIGAHE AWAHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA KWA USAHIHI FALSAFA YA KAIZEN

NAIBU WAZIRI KIGAHE AWAHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA KWA USAHIHI FALSAFA YA KAIZEN




DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe,  amewahimiza Watanzania kutumia kwa usahihi Falsafa ya Kaizen katika maeneo ya kazi ili  kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayodhamiria Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa juu wa kati unaoongozwa na ukuaji wa sekta ya viwanda.

Kigahe ameyasema hayo, alipokuwa Akimwakilisha Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Tatu ya Siku ya Kaizen Tanzania ambayo yalijumuisha utoaji wa tuzo kwa viwanda vilivyoshinda katika  Mashindano ya 6 ya  Kaizen kwa viwanda vinavyotekeleza falsafa hiyo, yaliyofanyika Februari 10, 2022  Dar es salaam .

Aidha, ameiomba Serikali ya Japan kupitia kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania, MShinichi Goto, kuendelea kufadhili mradi wa Kaizen ili kusambaza falsafa hiyo kuendana na utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Miaka 10 – “FKM 2020-2030” wa kueneza falsafa ya Kaizen pamoja  na kufikia hatua ya kuunganisha magari ya Japan nchini Tanzania. 

“Japan na Tanzania ni marafiki, sasa twende zaidi ya hapo; kwa kuwa sisi ndio wateja wenu wakubwa wa magari na Tanzania tumefikia uchumi wa kati. Ni muda mwafaka sasa sekta binafsi ya Tanzania na sekta binafsi ya Japan kufanya uunganishaji wa magari hapa nchini,” alisema Naibu Waziri na kuwasisitiza Watanzania kujiandaa vema kwa hilo kwa manufaa ya nchi zote mbili. 

Kigahe pia aliwashauri Watanzania kuzingatia ubora na kujikita katika ushindani ili Tanzania isiwe tu soko la bidhaa za nchi nyingine, bali Watanzania washiriki kwa viwango vya ubora wa hali ya juu katika soko likiwamo Eneo Huru la Biashara Afrika. 

Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yenye Kaulimbiu isemayo: “Kaizen! Kwa Tanzania ya Viwanda na Maendeleo Jumuishi!”  Balozi wa Japan nchini Tanzania, MShinichi Goto, alipongeza Tanzania kwa kukua kiuchumi licha ya changamoto zilizotokana na Covid-19 na kuitaka kutilia mkazo maendeleo ya biashara na viwanda vidogo na vya kati ili kukuza uchumi. 

Naye Mwakilishi Mkazi Mkuu wa JICA nchini Tanzania,  Naofumi Yamamura, alisema tangu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Bishara na JICA zishirikiane kutekeleza falsafa ya Kaizen, mwaka 2013 kuimarisha sekta ya viwanda, zaidi ya kampuni 100 nchini zinatekeleza falsafa hiyo na Watanzania 150 wamefuzu kuwa wakufunzi wa Kaizen.

Previous articleWIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWASILISHA TAARIFA YA HALI YA UJANGILI KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 11-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here