Home LOCAL ASKOFU JACKSON SOSTHENES WA ANGLIKANA AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SENSA YA WATU...

ASKOFU JACKSON SOSTHENES WA ANGLIKANA AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Na: Hughes Dugilo, DAR.

ASKOFU wa Kanisa Anglikana Dayosisi  ya Dar es Salaam Sossthenes  Jackson amewataka vijana wote nchini hasa wa kanisa hilo kujiandaa kikamilifu kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika Agosti mwaka huu.A

Ameyasema hayo leo Februari 5,2022 wakati kizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa semina Maalum ya Umoja wa Vijana wa kanisha hilo  Dayosisi ya Dar es Salaam (TAYO) iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Askafu Jackson amesema kuwa pamoja na mambo mengine ni vizuri vijana kutambua kuwa huu ni mwaka wa sensa Kitaifa, hivyo ni vema kuhamasishana wao kwa wao  kushiriki katika sensa hiyo kwani ni Jambo muhimu sana katika Taifa ambalo linawafanya watawala kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo .

Amesema uwepo wa sensa unafanya Serikali kujua idadi ya watu wake na vitu mbalimbali vilivyopo ambavyo vinazuzunguka jamii husika na kwamba Taifa lolote duniani linahitaji kujua idadi ya watu wake ili kupanga mipango yake ya kimaendeleo hivyo katika kufanikisha hilo kunahitajika uzalendo wa watu katika kujitokeza na kushiriki katika matukio muhimu  kama sensa.

“Tunafahamu Agosti mwaka huu nchi yetu inaingia kwenye jambo kubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili,tutakuwa na sensa ya watu na Makazi,niwaombe vijana wote nchini mkiwemo wa Kanisa la Anglikana kuhakikisha mnashiriki kwa vitendo, Serikali ikiwa na takwimu kamili ya watu wake pamoja na vitu vilivyopo ni rahisi kuweka mipango ya maendeleo,”amesema Askofu Jackson.

Ameongeza kwamba ipo changamoto ya baadhi ya vijana wa Kanisa kutokuwa wazalendo hata ndani ya Kanisa kwa kutosimamia vema kazi mbalimbali za Kanisa hilo wanazopatiwa, na kukemea vikali vitendo hivyo huku akisisitiza umuhii wa vIjanA hao kuwa wazalendo katika kutimiza majukumu yao ndani ya Kanisa na Taifa likiwemo kushiriki katika sensa.

Kuhusu semina hiyo Askofu Jacskon amewakumbusha vijana wote wa Kanisa hilo kuendelea kuwa waadilifu na wenye kujenga umoja,upendo na mshikamano katika jamii  inayowazunguka na Kanisa kwa ujumla huku akipongeza uongozi wa vijana hao Kwa kuandaa semina hiyo iliyoambatana na matukio mbalimbali likiwemo la kuliombea Taifa na viongozi wake.

Aidha semina hiyo imejenga msingi wa kuendelea kuwaleta  pamoja vijana wote kwa ajili ya kufungua mwaka mpya wa 2022 lakini pia kufanyika kwa Maombi ya pamoja kwa ajili ya Kanisa na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mratibu wa Umoja wa Vijana wa Kanisa hilo Padre Joseph Opiyo amewakumbusha vijana hao umuhimu wa kushiriki semina na makongamano yanayoandaliwa na Kanisa yenye lengo la kutambuana na kuwakumbusha majukumu yao katika Kanisa.

Pia amepata nafasi ya kuelezea kalenda ya Kanisa ya mwaka huu yenye matukio mbambali ya vijana ,na kwamba ushiriki wao kwenye matukio hayo kadrini muhimu. kulingana na kalenda inavyoelekeza.

Mwisho.

Previous articleTAKUKURU SINGIDA YAKAGUA MIRADI YENYE THAMANI YA SH. 1.2 BILIONI
Next articleVINARA WA LIGI KUU YANGA WASHIKWA KOO KWA MKAPA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here