Home SPORTS HITIMANA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

HITIMANA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

KAIMU Kocha Mkuu Hitimana Thiery  amesema kuwa amefurahishwa na kiwango walichoonyesha kiungo  mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

Ajibu aliingia kipindi cha pili na kuongeza ufundi katika idara ya ushambuliaji kwa kupiga pasi na kuwafungua  Namungo ambao muda mwingi walikuwa wanazuia.

Hitimana amesema Ajibu ni mchezaji mzuri ingawa hajapata nafasi kubwa ya kucheza lakini kuwa bado wana mechi nyingi na mashindano mbalimbali atazidi kuonekana uwanjani.

Ajibu ni mchezaji mzuri ana kipaji kikubwa tulimuingiza baada ya kuona Namungo wanacheza sana faulo na ajibu ni mzuri kwenye mipira ya adhabu tulijua atatusaidia na kweli  ametimiza malengo yetu” amesema.

Katika mchezo wa jana ajibu ndio aliyeanzisha mpira wa adhabu kwa Mohamed Husen ambaye alipiga krosi iliyounganishwa kwa kichwa na Medie Kagere na kutufungia bao la ushindi.

Previous articlePROF. MKUMBO ASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MAUZO YA NDANI SHANGHAI CHINA
Next articleNEMBO YA SWAHILI FASHION WEEK 2021 YAZINDULIWA RASMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here