Home LOCAL RC TABORA AAGIZA UTAFITI WA KINA WA MATUMIZI YA SALFA KWEMYE KOROSHO...

RC TABORA AAGIZA UTAFITI WA KINA WA MATUMIZI YA SALFA KWEMYE KOROSHO DHIDI YA MAENDELEO YA UFUGAJI WA NYUKI

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (aliyesimama) akitoa salamu za Serikali leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.

NA: TIGANYA VINCENT.

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amezitaka Taasisi za Utafiti wa wadudu kuchunguza matumizi ya salfa (sulfur) wakati wa kunyunyuzia  mikorosho  kama haina athari kwenye ufugaji nyuki.

Alisema ni kundi makundi ya nyuki yasije yakapotea kutokana na matumizi ya viwatilifu ikiwemo salfa ambavyo vinaweza kusababisha vifo kwa nyuki wakati wanakwenda kwenye maua kutafuta chavua.

Balozi Dkt. Batilda Buriani alitoa kauli hiyo leo wakati akihutubia kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.

Alisema asali ni nembo ya kielelezo kikubwa cha Mkoa wa Tabora kwa hiyo shughuli yoyote ya kuathiri makundi ya nyuki si vema ikafanyika.

Balozi Dkt. Batilda aliongeza kuwa nyuki wanazofaida nyingini ikiwemo uchavushaji mimea ya mazao mbalimbali na uzalishaji wa asali na mazao mbalimbali ya nyuki.

Balozi Dkt. Batilda alisema vitendo vya kuhatarisha maisha yao vinahatarisha pia maisha ya wakazi wa Tabora kwa kupoteza uatijiri wa asili wa asali na kuzodhfisha uzalishaji wa mazao mashamabani.

Alisema kimsingi hapingi ulimaji wa Korosho katika Mkoa huo bali kinachotakiwa kuangaliwa kwa upana faida na hasara zitakazopatikana kutokana na matumizi ya viwatilifu kwenye korosho dhidi ya uzalishaji wa asali.

Balozi Dkt. Batilda alisema ni vema watafiti wa wadudu na wale wa kilimo wakashirikiana ili kuja na msimamo wa aina moja katika suala la kilimo cha korosho Mkoani Tabora.

Alisema Mkoa huo uko katika mkakati mkubwa wa kuongeza matumizi ya mizingira kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa vitendo vya kuhatarisha maisha ya nyuki vitawarudisha nyuma.

Aidha Balozi Dkt. Batilda alisisitiza kuwa yapo mazao mengi ya kudumu nje ya korosho kama vile michikichi ambayo yakimwa Mkoani humo haya athari kwa nyuki.

mwisho.

Previous articleRAIS SAMIA AWASILI GLASGOW NCHINI SCOTLAND KUHUDHURIA MKUTANO WA 26
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU NOVEMBA 1-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here