Home BUSINESS MANDONGA MTU KAZI SASA ‘RASMI’

MANDONGA MTU KAZI SASA ‘RASMI’

Bw.Karim Mandonga (kulia) akikabidhiwa cheti cha Usajili wa Jina la Biashara na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Roida Andusamile, katika ofisi za BRELA, mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili mapema tarehe 15, Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), Bw. Goodluck Mushi (mwenye tai) akimpatia usaidizi wa usajili wa Jina la Biashara Bw. Karim Mandonga, alipofika katika Ofisi za BRELA tarehe 15 Novemba, 2022 kupata huduma na kusajili Jina la Biashara, Mandonga Entertainment.

DAR ES SALAAM 

Mwanamasumbwi ambaye amejipatia umaarufu katika siku za hivi karibuni, Bw. Karim Halid Mandonga , maarufu kwa jina la Mandonga Mtu Kazi, hatimaye amesajili jina la Biashara katika ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), baada ya kukamilisha taratibu za Usajili.

Akizungumzia hatua aliyofikia baada ya kukabidhiwa cheti cha Usajili wa jina la Biashara Mandonga Entertainment tarehe 15 Novemba, 2022 Bw. Mandonga amesema, inatokana na jitihada zilizofanywa na uongozi wa BRELA za kumhamashisha kusajili Jina la Biashara ambalo anaamini litamwezesha kufanya kazi zake bila ya kuwa na changamoto zozote.

Mandonga amesema kwa sasa yeye ni balozi wa BRELA na ataendelea kuwahamasisha wanamichezo wengine kurasimisha biashara zao kwani michezo ni biashara.

“Nimefurahi sana kupata cheti hiki kwani kitanipa ulinzi wa kisheria na biashara zangu zitakwenda vizuri”, amefafanua Bw. Mandonga.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akizingumza na Bw. Mandonga ofisini kwake amemtaka kutokukubali kutumika kirahisi na watu wenye nia ya kujinufaisha wao wenyewe.

Bw. Nyaisa amemsihi kuwasiliana na BRELA muda wowote kwa ushauri wa kibiashara ili kutimiza ndoto zake.

Previous articleSERA YA UBIA INAKWENDA KUIPA FURSA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA NYUMBA: MCHECHU
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 17-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here