Home LOCAL BALOZI MBAROUK APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO BALOZI MTEULE WA DRC

BALOZI MBAROUK APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO BALOZI MTEULE WA DRC

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini, Mhe. Jean-Pierre Massala katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara tarehe 15 Novemba, 2022 Jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea nakala hizo, Balozi Mbarouk amemhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali itampa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa Tanzania na DRC zitaendelea kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili hususan biashara na uwekezaji.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 16-2022
Next articleMRADI WA MAJI KIGAMBONI WALETA SULUHU UPATIKANAJI WA MAJI TEMEKE HADI KATIKATI YA JIJI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here