Home LOCAL WAZIRI MKUU RASMI MKUTANO WA KUMI WA WADAU WA LISHE

WAZIRI MKUU RASMI MKUTANO WA KUMI WA WADAU WA LISHE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 03, 2024 anafunga mkutano wa Kumi wa Wadau wa Lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malaika Beach Resort, Jijini Mwanza.

lengo la Mkutano huo ni kudumisha dhamira ya pamoja ya Serikali na wadau katika kuongeza msukumo na uwekezaji katika kutekeleza Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo katika jamii, na kupokea tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe nchini kwa mwaka uliopita.

Pia, Mkutano huo umelenga kutoa fursa kwa wadau wa lishe kukutana, kujadiliana na kupata maelezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 – 2025/26) uliouzinduliwa mwaka 2021.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni ”Kuchagiza Mchango Zaidi Wa Wadau Wa Kisekta Ili Kudumisha Matokeo Bora Ya Hali Ya Lishe Nchini Tanzania”

Previous articleTAARIFA YA KAMATI YA SERA YA FEDHA
Next articleRISE AND SHINE: THE HELLO JUA SUNRISE PARTY AT WAVUVI KAMPU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here