Home BUSINESS NHC KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

NHC KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linaendelea kujitanua katika utoaji wa huduma za makazi kwa Watanzania kwa kushiriki Maonyesho ya 7 ya Madini na Teknolojia yanayofanyika katika Viwanja vya EPZ, Bombambili, mjini Geita. Kupitia maonyesho haya, NHC inalenga kuwahamasisha Watanzania kujenga mustakabali wa maisha yao kwa kumiliki nyumba za bei nafuu na viwanja vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

Afisa Uhusiano wa NHC, Yamlihery Ndullah, akizungumza Oktoba 5, 2024, amesema kuwa shirika hilo limejizatiti kuwafikia wananchi kila kona ya Tanzania kwa kuwapatia fursa za kumiliki nyumba na viwanja kwa gharama nafuu. Alifafanua kuwa, miradi hiyo inapatikana katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Geita (eneo la Bombambili), Dodoma Iyumbu na mradi wa Samia Housing Scheme uliopo Kawe Jijini Dar es Salaam.

Ndullah alibainisha kuwa NHC si tu linajikita kwenye nyumba bali pia lina miradi ya maduka wanayopangishwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Nzongomela Kahama, Mtanda Lindi, Masasi Mtwara, na mpakani mwa Tanzania na Uganda Mtukula.

“Mikubwa kama Morocco Square, iliyopo makutano ya Morocco Jijini Dar es Salaam na Kawe 711, ni mfano wa uwekezaji mkubwa wa Shirika” amesema Ndullah.

Amesema kuwa Shirika hilo pia wanatekeleza mradi wa uuzaji viwanja katika eneo la Burka Mateves Jijini Arusha.

Aidha ametoa wito kwa wananchi mbalimbali kujitokeza kwenye maonesho hayo ili kupata taarifa zaidi na kushiriki furs muhimu wanazozitoa ikiwemo kumiliki nyumba na viwanja.

Kwa wale watakaoshindwa kufika, wanaweza kutembelea mitandao yao mbalimbali ya kijamii ili kupata huduma zaidi au kufika katika Ofisi zao za mikoa yote Tanzania bara.

Previous articleWADAU SEKTA YA ULINZI WAPEWA ELIMU
Next articleWAZIRI MKUU ASISITIZA MATUMIZI WA MIFUMO YA KIELOTRONIKI KATIKA MAKUSANYO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here