Home LOCAL WAZIRI CHANA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE BENKI YA DUNIA NA OFISI ZA...

WAZIRI CHANA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE BENKI YA DUNIA NA OFISI ZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Dodoma leo Septemba 5, 2024.

Ujumbe huo umekuja kumpatia mrejesho wa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia hasa katika uhifadhi wa maliasili na utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)ikizingatiwa kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana ameishukuru Benki ya Dunia kwa namna ambavyo imeendelea kuiwezesha Tanzania kwenye juhudi zake za uhifadhi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshugulikia maliasili, Kamishna Benedict Wakulyamba na Mratibu wa Mradi wa REGROW, Aenea Saanya.

 

Previous articleBRELA IMEFANYA KIKAO NA WADAU KUHUSU MKATABA WA SHERIA YA KIMATAIFA YA ULINZI WA MAUMBO NA MICHORO BUNIFU
Next articleJESHI LA POLISI LINATARAJIA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA JESHI LA POLISI TANZANIA  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here