Home BUSINESS SERA YA UBIA INAKWENDA KUIPA FURSA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA NYUMBA: MCHECHU

SERA YA UBIA INAKWENDA KUIPA FURSA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA NYUMBA: MCHECHU

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) Neemia Mchechu amesema kuwa kuzinduliwa kwa sera ya ubia kutawezesha utekelezaji wa  miradi mbalimbali kwa wakati inayosimamiwa na  shirika hilo.

Mchechu ameyasema hayo leo Novemba 16,2022 Jijini Dar es Salaam katika mahojiani na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sera ya ubia ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi.

Amesema sera hiyo itasaidia kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya nchi pamoja na kuchochea kuongezeka kwa kasi ya ujenzi wa nyumba kwa lengo la kupunguza mahitaji ya nyumba nchini.

“Sera hii inakwenda kuamsha uwekezaji mkubwa hapa nchini pamoja na kutia hamasa mpya katika kupunguza mahitaji ya nyumba nchini kutokana na Sekta Binafsi kuweza kupata maeneo ya uwekezaji kiurahisi”

“Pia Sera itatoa fursa kwa NHC kuingia ubia na Sekta Binafsi kujenga miradi ya maendeleo katika viwanja vinavyomilikiwa na Shirika” amesema Mchechu.

Aidha ameongeza hatua hiyo inaunga mkono maelekezo ya Rais Samia Suluhu kuruhusu Sekta Binafsi kuwekeza mitaji ili kujenga uchumi wa Taifa.

Previous articleMAKAMU MWENYEKITI WA CTI HUSSEIN SUFIAN AZUNGUNZIA TUZO ZA RAIS KWA MZALISHAJI BORA WA MWAKA (PMAYA) KWA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR
Next articleMANDONGA MTU KAZI SASA ‘RASMI’
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here