Home BUSINESS KAIMU KATIBU MKUU GUGU AONGOZA KIKAO CHA 6 CHA TNBC JIJINI DAR

KAIMU KATIBU MKUU GUGU AONGOZA KIKAO CHA 6 CHA TNBC JIJINI DAR

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu tar 17 Novemba, 2022 ameongoza kikao Kazi cha sita cha Tanzania National Business Council (TNBC) kwa lengo la kujadili na kupokea mapendekezo ya maboresho ya rasimu ya itifaki ya Viwanda ya SADC (SADC Industrial Protocol) kabla ya Serikali kuridhia na kuanza utekelezaji wa itifaki hiyo.

Pamoja na kujadili Itifaki hiyo, wajumbe wa Kikosi Kazi cha TNBC walijadili changamoto, fursa na maboresho katika sekta ya Viwanda Nchini.

Mkutano huu umehudhuriwa pia na Katibu Mtendaji wa TNBC Bw. Godwil Wanga, Mwenyekiti Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) Bw. Paul Makanza, Mwenyekiti TEGAMAT Bw. Adam Zuki pamoja na ujumbe kutoka Zanzibar ukiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Dkt. Abdallah R. Abdallah.

Previous articleDKT. KIJAJI AZITAKA TAASISI ZA FEDHA NCHINI KUTOA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU
Next articleTANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA TAWI JIPYA KUFANYA KAZI SAA 24
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here