Home SPORTS KAGERE AIBEBA SIMBA.

KAGERE AIBEBA SIMBA.


Na: Stella Kessy DAR ES SALAAM.

MABINGWA watetezi Simba leo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa dimba la Benjamini Mkapa.

Bao la dakika ya mwisho lililofungw na Mshambuliaji meddie Kagere limetosha kuwapatia point 3 Simba.

Kagere aliyetokea benchi alifunga bao hilo kwa kichwa cha chini chini baada ya kumalizia  mpira krosi uliopigwa na Mohamed Husen kufuatia shambulizi lililoanzia kwa Ibrahim Ajib.

Dakika 15 za kwanza kikosi cha simba kilianza kwa kasi kwa kuandama lango la Namungo na dakika ya tisa Benard Morison alikosa bao  baada ya kazi nzuri ya Kibu Denis hata hivyo pasi ilienda pembeni.

Hata hivyo katika dakika ya 51 kiungo mkabaji wa Namungo Abdulaziz Makame alionyeshwa kadi nyekundi baada ya kimvhezea madhambi Shomari Kapombe.

Hata hivyo Kocha mkuu Hitimana Thiery aliwatoa Morrison,Yusuph Mhilu na Bocco na kuwaingiza  Ajibu, Duncan Nyoni na Kagere ambao walionuesha tofauti mchezoni.

Ushindi wa leo utawafanya simba kufika alama 11 baada ya kushuka dimbani mara tano kwa msimu huu.

Previous articleRC MAKALLA: MABORESHO YA COCO BEACH YAMELENGA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NA UBORESHAJI HUDUMA.
Next articleKUTOKA MAGAZETI I ALHAMISI YA LEO NOVEMBA 4-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here