Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela
Mratibu wa mradi wa CLARITY Redman Mjema
Baadhi ya wadau wa mashirika yasiyokuwa ya Ku serikali ( NGO’s) Mkoa wa Geita.
Na. Costantine James, Geita.
Mratibu wa Mradi wa CLARITY Kupitia Shirika la kimataifa la kujitolea (VSO) Redman Mjema amesema Shirika hilo linatekeleza mradi huo wenye lengo la kusimamia haki za binadamu na ulinzi na usalama wa mazingira katika Mkoa wa Geita na Mara.
Amesema Mradi huo umejikitika katika kusimamia haki za binadamu katika mazingira yenye uchimbaji wa madini pamoja utunzaji wa mazingira.
Amesema kupitia mradi wa CLARITY wanatoa mafunzo kwa viongozi pamoja na taasisisi mbalimbali kwa lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto Mkoani Geita pamoja na kutokomeza utumikishwaji wa watoto hasa maeneo ya migodini.
Mku wa Mkoa wa Geita Martine Shigela wakati akizungumza kwenye Mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s) ulifanyika katika ukumbiwa EPZA Bombambili amezitaka Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGOs) kuungana kwa lengo la kudhibiti utumikishwaji wa watoto hasa kwenye maeneo ya migodini.
Shigela amesema mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yananafasi kubwa katika kusaidiana na serikali kutokomeza utumikishaji wa watoto katika maeneo mbalimbali hasa migodini.
Shigela amesema tatizo la ajira za watoto linatishia usalama wao na hata kupelekea watoto hao kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu na kupelekea ongezeko la watoto wanaokatisha masomo .
Amesema ipo haja ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuungana kwa pamoja kuliangalia tatizo hilo na kuja na suluhisho la kudumu kuweza kuokoa watoto kutokimbilia hasa maeneo ya migodini na kuwasaidia waendelee na masomo ili kuzalisha wasomi hapa nchini.
“wakati mwingine watoto wadogo badala ya kwenda kusoma na kunufaika na elimu bila malipo shuleni lakini watoto wadogo wanatumikishwa kwenye migodi kwa hiyo sisi asasi za kiraia ni wajibu wetu kufuatilia mambo kama haya Ili tuweze kuyakomesha watoto wetu wasome waje kulifaa taifa kwa kazi ambazo zitakuwa zinapatikana ndani ya taifa letu kwa hiyo nataka niwaombe na kuwasihi kushiriki kikamirifu.” Amesema Shigela.