Na: Mwandishi wetu.
Klabu ya soka ya wekundu wa msimbazi Simba SC leo imetoshana nguvu na timu ya KMC kwa kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa ligi Kuu ya NBC.
Katika mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam timu ya Simba ilikuwa ya kwanza kuliona lango la KMC kwa goli la kuongoza likifungwa na mshambuliaji wake wa Kimataifa Moses Phil dakika za mwanzoni mwa mchezo huo.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Simba ilikuwa ikiongoza kwa bao hilo huku timu zote zikionekana kuwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kasi na mnamo dakika ya 47 kiungo mshambuliaji wa KMC Mateo Anthony alipachika bao la kusawazisha.
Katika dakika ya 58 ya mchezo huo George Makanga alipachika bao la pili ambapo Simba walisawazisha katika dakika za lala salama za mchezo huo goli likifungwa na mshambuliaji wake Abib kyombo.
Kufuatia matokeo hayo Kila timu imeondoka na alama 1 huku Simba ikikusanya jumla ya alama 7 na magoli 7 zinazowafanya kukaa juu ya uongozi wa ligi.