Afisa lishe kutoka TAHA Salome Stephen (kushoto) na Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka TAHA Magdalene Mhina (kulia) wakionyesha Mazao ya Sltrucurture. |
Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka TAHA Magdalene Mhina akitoa maelezo kwa mgeni alifika kwenye Banda lao. |
Afisa Utawala TAHA Morogoro Philemon Mduma (kulia) akiwahudumia wananchi waliofika kwenye Banda lao kujifunza Mambo mbalimbali ya Taasisi hiyo. |
Afisa Uhusiano kwa Wateja wa TAHA Lovennes Adolf Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. |
Watanzania hususani Vijana wameshauriwa kufanya kilimo cha Biashara kitakachoweza kuwahakikishia kupata kipato cha uhakika na kuendesha maisha yao.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano kwa Wateja wa Shirika hilo Lovennes Adolf alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa (Sabasaba) ambapo amesema kuwa TAHA wamekuwa jukwaa la kutoa sauti kwa wazalishaji, wafanyabiashara, wauzaji bidhaa pamoja na wasindikaji wa mazao ya horticulture na kwa kwamba wakulima waliopo chini ya Taasisi hiyo wameweza kunufaika kwa kiasi kikubwa na kilimo hicho.
“Ndugu zangu wanahabari TAHA Tunatekeleza shughuli zetu kupitia mfumo wa kongani kama sehemu ya kufikia jamii ambazo zimelengwa kikamilifu hivi sasa, Amesema Lovennes.
Akizungumzia maonesho hayo amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maonesho na ushiriki wao umeweza kusaidia kukutana na wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakifika kutaka kufahamu shughuli za TAHA.
Amefafanua kuwa matumaini yao kama TAHA baada ya kumalizika kwa maonesho hayo watakuwa wamepata mabalozi wazuri ambao watakuwa mstari wa mbele kuitangaza Taasisi hiyo.
“Hii ni fursa kubwa kwani baada ya maonesho haya tunaamini kila aliyepita hapa atakuwa Ballozi mzuri wa kuitangaza Taasisi yetu. Ameongeza