Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda, ametembelea katika Mnada wa Old Shinyanga, kutoa elimu na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu.
Akizungumza na wananchi kwenye mnada huo, amewasihi siku hiyo ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu, washiriki kikamilifu , ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo kuanzia ngazi ya chini.
“Tunaendesha zoezi la Sensa ya watu na makazi ili tujue Tanzania tuko watu wangapi, na itaisaidia Serikali katika upangaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wote kulingana na idadi yao,” amesema Makinda.
“Rais Samia Suluhu Hassani amekuwa akitafuta fedha za maendeleo kwa wananachi wake, na anataka kujua ni maeneo gani ambayo wananchi bado hawana maendeleo kwa uwiano sawa na idadi yao, hivyo nawasihi jitokezeni kuhesabiwa Sensa,” ameongeza.
Aidha, amewataka pia wananchi watoe ushirikiano kwa Makarani wakati wa Sensa pamoja na kutoa taarifa za kweli na usahihi na siyo kudanganya ili siku huduma zikianza kutolewa na Serikali katika eneo husika kusiwepo na mapungufu.
“Kama wewe una ng’ombe 100 wataje wote usiseme una ng’ombe 10, ili siku madawa yakija kulingana na idadi ya mifugo mlioitaja msianze kugombania na kulalamika madawa hayatoshi na wakati awali nyie ndiyo mlitoa taarifa siyo sahihi,” amesema Makinda.
Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wasiwafiche ndani watu wenye ulemavu pamoja na wazee, bali wawape fursa nao ya kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa.
Nao baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mnada huo pamoja na wafanyabiashara, wameshukuru kupatiwa elimu hiyo kuhusu Sensa ya Watu na Makazi.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa ya watu na makazi kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agost 23 mwaka huu.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Pastory Ulimali akizungumza kwenye Mnada huo wa Old Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza na wananchi kwenye Mnada huo wa Old Shinyanga wakati wa utolewaji wa elimu ya Sensa.
Wananchi wakisikiliza elimu ya Sensa na kuhamasishwa washiriki kuhesabiwa Agosti 23 mwaka huu.
Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya Sensa.
Elimu ya Sensa ikiendelea.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Olshinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agost 23 mwaka huu.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA