Home BUSINESS KUELEKEA KILELE CHA KUPINGA BIDHAA BANDIA, WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUZITUMIA

KUELEKEA KILELE CHA KUPINGA BIDHAA BANDIA, WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUZITUMIA

DAR ES SALAAM 

WANANCHI wametakiwa kuacha mara moja matumizi ya bidhaa bandia na badala yake kuhakikisha kuwa wanatumia bidhaa halisi hali itakayosaidia kuchochea uwekezaji, kukuza fursa za ajira na hatimaye kuchagiza ukuaji wa uchumi wao na Tifa kwa ujumla

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya kupinga na kudhibiti bidhaa bandia Duniani , ambayo kilele chake kitakuwa kesho Julai 18,2024 Jijini  humo.

Amesema kuwa kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara zinayofanyika ulimwenguni zinahusisha bidhaa bandia na kubainisha kuwa baadhi ya madhara ya bidhaa hizo ni pamoja na kutopata thamani halisi ya fedha pamoja na madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji

Kadhalika amewataka wafanyabiashara nchini kuacha kuagiza ama kuuza bidhaa bandia kwani kwa kufanya hivyo wanashusha ushindani wa kibiashara sambamba na kupoteza mapato ya serikali hivyo tume imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusiana na madhara hayo

Maadhimisho hayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo “Kudumisha uhalisia kwa kulinda ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini” ambapo yanafanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Previous articleSHIRIKA LA POSTA LAPONGEZWA KWA MASHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI
Next articleRAIS SAMIA AKITETA JAMBO NA WAZIRI BASHE AKIWA ZIARANI RUKWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here