Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Wizara ya Fedha imeibuka Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Aidha, Taasisi yake ya Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi (PPRA) imeshika nafasi ya Kwanza kwa Upande wa Mamlaka za Udhibiti nchini, huku Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA), ikishika nafasi ya Pili katika kundi la Taasisi za Serikali
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, akiitazama Tuzo ya ushindi wa pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba na Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Bi. Lilian Rugaitika, wakiwa wameshika Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yalifanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, baada ya Wizara ya Fedha kuibuka na Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoandaliwa na TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Timu ya ushindi kutoka Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha, wakishangilia Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (IAA) baada ya Wizara ya Fedha kushinda Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Kinondoni, wakishiriki kwa furaha ushindi wa Wizara ya Fedha baada ya kuibuka Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024.
Picha ya Tuzo ya Mshindi wa Pili wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ya TANTRADE (Sabasaba), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam, mwaka 2024, ambapo Wizara ya Fedha imekabidhiwa Tuzo hiyo baada kushinda nafasi ya Pili ya Banda Bora katika Maonesho hayo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)