Na.:Costantine James, Geita.
Waziri wa madini mhe, Dkt. Dotto Biteko amewataka waumini wa kanisa la africa Inland Church Tanzania (AICT) dayosisi ya kalangalala Mkoani Geita kuiombea nchi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan Kwani nchi haiwezi kusimama bila maombi ya watakatifu pamoja na waumini wa dini mbalimbali.
Mhe, Dkt. Dotto Biteko ametoa Rai hiyo leo tarehe 10.7.2022 mkoani Geita wakati wa hafra ya uwekaji wakfu katika kanisa la africa Inland Church Tanzania (AICT Kalangalala) amesema watanzania kwa ujumla wanapaswa kuiombea nchi ili iwe na amani na usalama.
Waziri Dkt. Biteko amesema waamini wanapaswa kuliheshimu kanisa ikiwa ni pamoja na kufata sheria na kanuni za kanisa amewataka pia wazazi kuwafunza watoto kumpenda mungu ili wakue na maadili mema kwa lengo la kujenga taifa bora la kesho.
Amesema watoto wakilelewa katika misingi ya dini itawawezesha kukuwa vyema nakuwafanya wasijihusishe na mambo maovu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, wizi na mambo mengine ya kidunia.
Waziri Biteko ametumia nafasi hiyo kuzitaka pia taasisi za kidini nchini kuisaidia serikali kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto unaondelea kushamiri kwenye maeneo tofauti hapa nchini.
Askofu Mkuu wa AICT, Askofu Mussa Magwesela amewataka wakazi wa Geita na Tanzania kwa ujumla kujitoa katika shughuli mbalimbali za kanisa kuunga mkono ujenzi wa nyumba za ibaada kwani zina mchango mkubwa katika kuimarisha maadili na kupiga vita vitendo viovu.
Amesema nyumba za ibada zikitumika vyema kuielimisha jamii juu ya maswala ya ukatili wa kijinsia zinanafi kubwa katika kuchangia kukemea maovu ambayo yanatokea katika jamii pamoja na kuchangia kuleta amani kwa jamii.
Naye Mbunge wa Jimbo la Geita mjini, Mhe Constantine Kanyasu amekiri kuwa endapo viongozi wa dini watasimama imara katika kukemea ukatili ndani ya mkoa wa Geita na maeneo mengine wataweza kuishinda vita dhidi ya ukatili.
Amesema ni Kweli hivi kalibuni kumekuwa na Matukio ya ukatili na matukio mengi yanahusianishwa na imani za kishirikina ameziomba taasisi za kidini kutoka nje makanisa kwajili ya kwenda kuwahubilia wananchi ambao bado hawamjui mungu kwani kufanya hivyo kutapunguza matukio ya ukatili katika jamii.