Na: Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jumla ya watoto watatu wa kiume wamezaliwa katika mkesha wa Krismasi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa salama wenye afya njema.
Akizungumza afisa muuguzi msaidizi kiongozi wa wodi ya wazazi Experantia Misalaba amesema jumla ya akina mama watatu wamejifungua wawili kati yao kwa njia ya upasuaji na mmoja amejifungua kwa njia ya kawaida na kwamba wote wamezaliwa salama wakiwa na uzito wa kawaida.
“Hospitali yetu ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga katika siku ya sikukuu yetu ya leo ya Krismasi tumefanikiwa kupata wakinamama watatu waliojifungua wakina mama wawili wamejifungua kwa upasuaji na mama mmoja amejifungua kwa njia ya kawaida tumepata watoto wote niwajinsia ya kiume watoto wawili wana kilo 2.8 na mmoja ana kilo 3.5 na watoto wote hao wako salama”.
Muuguzi huyo amewaomba wazazi na walezi kufurahi na kusherehekea sikukuu ya Krismasi pamoja na watoto na familia zao.
“Kwa sababu ni sikukuu ya familia pamoja wazazi na watoto wao tunawaomba wakina mama wote leo washerehekee sherehe hii pamoja na watoto wao kwa sababu ni siku ya kuzaliwa kristo ni pamoja na watoto kufufuka”.
Mmoja wa akina mama waliojifungua katika mkesha wa Krismasi Bi. Lightiness Kadala mkazi wa Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga amemshukuru mwenyezi Mungu kwa kujifungua salama katika mkesha wa sikukuu ya Krismasi.
“Nimejisia vizuri sana kwa sababu yesu amezaliwa nimejifungua mtoto wa kiume nimemuita jina lake Emmanuel kwa furaha zote nilizokuwa nazo namshukuru sana Mungu maana haijawahi kutokea ila ni neema tu ya mwenyezi Mungu ni historia pia katika maisha yangu na nilitamani sana iwe hivyo nilikuwa namuomba sana Mungu na kweli imekuwa hivyo nimejifungua tarehe hiyohiyo ni jambo kubwa sana la neema kwangu”.
Afisa muunguzi msaidizi kiongozi wa wodi ya wazazi Experantia Misalaba ametumia nafasi hiyo kuiomba jamii kufika katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kupata vipimo, huduma ya matibabu kutoka kwa watalaam waliobobea.