Na: Hughes Dugilo, MOROGORO
Imeelezwa kuwa uwepo wa dhana ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi unaweza kuwa na manufaa makubwa kwa Serikali, kama ilivyo kwa Sekta Binafi, nakwamba jambo hilo ni la msingi kwa maendeleo ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, wakati akifungua semina ya siku moja ya utoaji wa elimu kuhusu usimamizi wa mnyororo wa ugavi kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni, iliyofanyika leo Juni 18, 2025 mkoani Morogoro .
Mwakibinga amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti yake katika ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa ajili ya wananchi.
Aidha amebainisha kuwa kutokuwepo kwa usimamizi thabiti wa shughuli zilizopo katika mnyororo wa Ugavi, unaweza kuleta athari kubwa, nakwamba kwa kuzitambua athari zinazoweza kujitokeza kutakuwa na mazingira mazuri ya kutengeneza miongozo na mikakati mbalimbali ili kuhepukana na athali hizo.
“Ni vizuri sana kutambua athali za kutokuwepo kwa usimamizi thabiti wa shughuli zilizopo katika mnyororo wa Ugavi, kwani ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa.
“kwa kuzitambua athari zilizopo tunaweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kutengeneza miongozo na mikakati mbalimbali ya utekelezaji, ili kuimarisha usimamizi wa utekelezaji na kuhepukana na athali hizo” amesema Dkt. Mwakibinga.
Aidha, DKt. Mwakibinga alitolea mfano wa bajeti ya mwaka 2024/2025, ambayo ilikuwa shilingi trilioni 50.29, ambapo zaidi ya trilioni 35.2 zilitengwa kwa ajili ya manunuzi ya huduma na bidhaa, nakwamba endapo mnyororo huo hautosimamiwa vizuri, kuna hatari ya fedha hizo kuvuja na kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
“Kama muunganiko wa mnyororo wa ugavi hautakaa vizuri, fedha ambazo zimebadilishwa kuwa huduma au bidhaa zitavuja njiani. Hilo sio lengo. Lengo ni kuhakikisha thamani ya fedha hizo inamfikia mwananchi,”