Home LOCAL NHC YAWEKA REKODI YA UKUAJI MZURI WA FEDHA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

NHC YAWEKA REKODI YA UKUAJI MZURI WA FEDHA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

DAR ES SALAAM 

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeweka rekodi ya ukuaji mzuri wa fedha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kuongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 125 mwaka 2019 hadi 189 bilioni mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko kubwa la asilimia 33.1.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Hamadi Abdallah Hamad, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari leo June 16, 2025, Jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea miradi minne inayotekelezwa na Shirika hilo.

Hamad ameeleza kuwa Ukuaji huo ni matokeo ya uwekezaji wa kimkakati, na dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya upatikanaji wa nyumba za bei nafuu na kuboresha sekta ya makazi hapa nchini.

“Ukuaji huu wa ajabu ni matokeo ya uwekezaji wa kimkakati, uboreshaji na dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, nchini kote,” alisema Hamad.

Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano, NHC ilikusanya jumla ya Shilingi Bilioni 235.4, huku faida ikiongezeka sambamba na mapato ya asilimia 33.1 nakupelekea kuwepo kwa ongezeko kubwa la Gawio kwa serikali ikipanda kutoka Shilingi Milioni 550 mwaka 2019 hadi Bilioni 5.5 mwaka 2024, huku akibainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2023 na Juni 2024 pekee, NHC ilikusanya kodi ya Shiling Bilioni 36.8, na kupita lengo lake la mwaka kwa kufikia asilimia 112.5.

Lengo letu kwa mwaka ujao wa fedha ni TZS 10 bilioni, na ninaamini tunaweza kulifikia,” ameongeza.

Ili kuendeleza kasi hiyo, Hamad ametangaza kuwa NHC inapanga kuingia katika masoko ya mitaji kwa kuzindua hati fungani ya miaka saba katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ikiitwa Nyumba Bond, kwa lengo la kukusanya fedha za kukamilisha miradi ya kimkakati ya ujenzi wa nyumba, hasa zile zilizo chini ya Mpango wa Samia Housing Scheme, ifikapo 2030.

Ziara hii ya Wahariri wa vyombo vya Habari, imewapa fursa ya kujionea uendelezwaji wa Miradi mikubwa ya Samia Housing Scheme (SHS), Kawe 711,Golder Premier (GPR), na Morocco Square yote ya jijini Dar es Salaam, iliyopo chini ya NHC.