DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama amesema wote wanaomsema vibaya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani kwa kufanya hivyo wanamsema Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyempa Mamlaka aliyonayo.
Msama ametumia vifungu vya Bibilia kutoka katika Kitabu cha Warumi 13:3 -1 akinukuu, “Kila mtu atii Mamlaka Kuu, Kwa maana hakuna Mamlaka isiyotoka kwa Mungu” hivyo kuwasihi Wananchi wote kuheshimu Mamlaka ambazo zinawaongoza.
Ameyasema hayo Leo Juni, 8, 2025 Jijini Dar-es-Salaam, wakati Akizungumza na waandishiwa habari, na akifafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameteuliwa na Mungu kwaajili ya kuwatumikia Watanzania.
Aliongeza kuwa, kwa sasa Rais Samia anakaribia kumaliza kipindi chake, akitarajia kuingia kwenye awamu ya pili. hivto ni muhimu kwa wananchi, hususani wale wanaojihusisha na dini, kumheshimu Rais na mamlaka zake.


