
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe Japhari Kubecha Ameshiriki Uboreshaji wa Taarifa zake Kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Leo Mei 21, 2025 Katika Kituo Kilichopo Kata ya Vibaoni.
Mhe Kubecha Ametoa wito kwa Wakazi wa Handeni Kushiriki Uboreshaji wa Taarifa zao Kwenye Daftari Hilo, La Kujiandikisha au Kuboresha Taarifa zao za Awali, Ni Muhimu Wananchi wa Handeni Kujitokeza kwa Wingi Kushiriki Kuboresha Taarifa Zao au Kujiandikisha.
Tunafahamu Mwezi Oktoba Kutakuwa na Uchaguzi Mkuu Ambapo Tunakwenda Kuchagua Madiwani, Wabunge pamoja na Rais ,Kwahiyo Ili Kupata Haki Yako ya Msingi Basi ni Lazima Ujiandikishe au Kuboresha Taarifa zako ili Uweze Kupata Haki ya Msingi ya Kikatiba Kuchagua Viongozi Hao, Aidha Niwaombe Viongozi wa Dini Kuhamasisha Waumini Kujitokeza kwenye Zoezi Hili Muhimu Ambapo Mwisho Ni Kesho Tarehe 22 Mwezi Mei.
.jpeg)


