Home LOCAL GAVANA BWANKU ATUMIA MKUTANO WA KIJIJI RWAGATI KUHIMIZA WANANCHI KULINDA AMANI KWENYE...

GAVANA BWANKU ATUMIA MKUTANO WA KIJIJI RWAGATI KUHIMIZA WANANCHI KULINDA AMANI KWENYE MWAKA HUU WA UCHAGUZI

_Awahakikishia Wananchi kwamba Uchaguzi upo mwaka huu 2025, awaeleza miradi mikubwa iliyotekelezwa na Serikali ya Rais Samia kwenye Kata yao ya Kemondo._

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Jana Alhamisi Aprili 10, 2025 Kijiji cha Rwagati kilichopo Kata ya Kemondo kimefanya Mkutano Mkuu wa Kijiji ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji Ndugu Yahya Nuru na kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama, masuala ya maendeleo, changamoto za wananchi huku Wataalamu wa kilimo na mifugo, maendeleo ya jamii, afya, jeshi la polisi na wengine wakitoa ufafanuzi kwa wananchi wa masuala mbalimbali.

Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku ameshiriki Mkutano Mkuu huo wa Kijiji ambapo kwenye salamu zake kwa wananchi baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza amesisitiza wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kulinda amani na usalama wa maeneo yao kwa kuripoti kila viashiria vya uvunjifu wa amani hasa mwaka huu ambao Taifa litafanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Gavana Bwanku amewahakikishia wananchi wote kwenye mkutano huo kwamba Uchaguzi Mkuu utafanyika mwaka huu kama Katiba ya Nchi inavyosema huku akiwasisitiza wananchi kujipanga kuchagua viongozi bora wa kusaidiana nao kusukuma maendeleo.

Aidha, Gavana Bwanku alitumia mkutano huo kuwaeleza wananchi jinsi Kata yao ilivyopata miradi mingi na mikubwa ya maendeleo kwa muda mfupi wa miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Kata hii imepata Bilioni 20 ya upanuzi wa Bandari ya Kemondo, Bilioni 15.8 kwa mradi mkubwa wa maji Kemondo, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ambavyo vyote vimejengwa kata hii na shughuli zote za utawala wa Halmashauri zinapatikana kata hii.

Pia, Kata hii miaka hii 4 ya Rais Samia imepata ujenzi wa shule mpya ya kisasa ya msingi ya Kanazi B milioni 540, milioni 100 kwa taa za barabarani, milioni 17.3 kwa ukarabati wa mwalo wa samaki Rushala kwenye Ziwa Victoria na mengine mengi sana huku Serikali ikitenga zaidi ya milioni 500 kujenga soko la kisasa la ndizi Kemondo, ghala la dagaa, ukumbi na kuiboresha stendi ya Kemondo.

Gavana Bwanku alisisitiza viongozi kwenda kuyasemea haya kwa wananchi ili wajue kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa kwenye maeneo yao.