Home LOCAL ZOEZI LA UOKOAJI LIWE ENDELEVU-MAJALIWA

ZOEZI LA UOKOAJI LIWE ENDELEVU-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 18, 2024 amekagua muendelezo wa zoezi la uokoaji katika jengo lililodondoka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam na amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi atakapotolewa mtu wa mwisho aliyekwama kwenye jengo hilo.

Aidha Mheshimiwa Majaliwa amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamtafuta mmiliki wa jengo hilo ili aweze kusaidia kufahamu juu ya chanzo cha kudondoka kwa jengo hilo.

Pia ametoa wito wa watanzania kuacha kuchangisha Watanzania kwani Serikali inaoutaratibu wa utoaji wa misaada kupitia Kamati ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Previous articleMCHUMBA WANGU ALITUPIWA JINI NA NDUGU ZAKE ILI NISIMUOE
Next articleBASHUNGWA AIAGIZA TANROADS KUFUNGA MIZANI MITATU YA KUPIMA UZITO WA MAGARI TUNDUMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here