Home LOCAL TANZANIA NA PAKISTAN KUENDELEZA USHIRIKIANO

TANZANIA NA PAKISTAN KUENDELEZA USHIRIKIANO

Kaimu Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Marcus Mbilinyi alifanya mazungumzo na Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Mhe. Siraj Ahmed Khan jijini Dar Es Salaam Juni 24, 2024.

Wakati wa mazungumzo hayo viongozi hao walisaini Muhtasari wa Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Pakistan (Agreed Minutes of the Bilateral Political Consultations-BPC).

Makubaliano hayo ambayo majadiliano yake yalifanyika mwezi Machi 2024 yaligusia ushirikiano kwenye biashara; uwekezaji; elimu; sayansi, teknolojia; mafunzo ya kujengeana uwezo; ulinzi, usalama; utamaduni na masuala ya kikonseli.

Kwa ujumla Makubaliano hayo yalilenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kwa faida na mustakabali bora wa nchi hizi mbili.

Previous articleNHC INAVYOKWENDA KUGEUZA ENEO LA URAFIKI KISASA
Next articleMTATURU AISHAURI SERIKALI KUONDOA URASIMU KWENYE BIASHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here